Mamlaka ya jimbo la Sudan kusini la Unity imesema kuwa takriban watu 7 wamekufa baada ya mafuriko kusomba nyumba zao kwenye eneo la Mayendit huku familia takriban 400 zikilazimika kuhama makwao katika siku za karibuni.
Mkuu wa kaunti ya Mayendit, Gatluak Nyang Jumatatu ameambia VOA kipindi cha South Sudan in Focus, kwamba mvua kubwa zimeendelea kunyesha katika wiki kadhaa zilizopita. Watu hao 7 wanasemekana kufa maji kutokana na mafuriko huko wengine 17 wakisemekana kuumwa na nyoka,Nyang ameonegeza kusema.
Amesema pia kwamba takriban asilimia 90 ya ardhi ya Mayendit imefunikwa na maji ambayo pia yameuwa zaidi ya ng’ombe 500 na mbuzi 300. Nyang anasema kuwa watu wengi wanateseka kutokana na magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa mazingira safi, pamoja na malaria kutokana na kuwa hawana neti za kujikinga na mbu.
Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yameombwa kuingilia kati na kupeleka misaada muhimu ya kibinadamu.
Ndege zikiwa kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow Uingereza
Uingereza Jumatatu imefungua mipaka yake kwa watu waliopewa chanjo kamili ya covid kutoka Marekani na kwenye mataifa kadhaa ya bara Ulaya, wakati serikali inapojitahidi kurejesha hali ya kawaida ya maisha.
Hata hivyo wanaoingia nchini lazima wapimwe corona kabla ya kuingia ndege, na pia wapimwe tena siku mbili baada ya kuingia nchini humo, japo sasa hawatawekwa kwenye karantini kama ilivyokuwa hapo awali.
Watu kutoka Ufaransa hata hivyo wataendelea kuwekwa kwenye karantini baada ya kuwasili Uingereza kutoka na idadi kubwa ya maambukizi ya aina mpya ya virusi vya beta nchini humo, vilivyo gunduliwa kwa mara ya kwanza Afrika kusini.
Uingereza ni mojawapo ya mataifa yanayoongoza katika utoaji wa chanjo za covid ikisemekana kuwa karibu asilimia 90 ya watu wazima nchini humo tayari wamepokea walau chanjo ya kwanza. Taifa hilo limepanga kuanza kutoa chanjo ya tatu maarufu kama booster, kwa wakazi wake milioni 32 hapo mwezi Septemba.
Freeman Mbowe, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Dar es Salaam, Tanzania. Ericky Boniphace AFP/Archivos
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema halitakubali maandamano ya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, wakati kiongozi wao Freeman Mbowe atakapofikishwa tena Mahakama siku ya Alhamisi kwa madai ya ugaidi.
« Jeshi la polisi linatoa onyo kwa mtu au kikundi cha watu kitakachojaribu kuhamasisha mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana au namna yoyote ile kutoa shinikizo lolote, » amesema Simon Sirro,Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika alitangaza kuwa wafausi wa chama hicho washiriki kwenye maandamano ya amani kote nchini humo, kupinga mashtaka dhidi ya Mbowe ambayo chama chake kinasema ni ya uongo.
Madaktari nchini Nigeria wanaofanya kazi kwenye hopsitali za umma, wameanza mgomo usiogoma kudai nyongeza ya mshahara, bima ya afya na kulalamikia ukosefu wa vifaa kwenye vituo vya afya.
Rais wa chama cha Madaktari nchini humo Uyilawa Okhuaihesuyi ametangaza kuwa mgomo huo haujulikani utaisha lini.
Madaktari wamesisitiza kuwa, hawapo tayari kurejea kazini hata kwa wale wanaoshughulikia maambukizi ya Covid 19, wakati huu Madakatari wengine 19 wakipoteza maisha kutokana na virusi hivyo.
Nchini Rwanda, malengo ya chanjo bado hayajafikiwa. Ludovic MARIN AFP/File
Rwanda inajaribu kudhibiti mlipuko wa tatu wa gonjwa la Covid-19. Katika wiki za hivi karibuni, nchi hiyo imerekodi kati ya kesi 500 na 1,000 za kila siku, takwimu ambazo hazijawahi kufikiwa. Hii ilisababisha serikali kutangaza katikati ya mwezi Julai marufuku kwa mara ya tatu ya watu kutotembea tangu kuzuka kwa janga hilo nchi humo.
Serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba marufuku hiyo itadumu wiki mbili, wakati katika mji wa Kigali na katika wilaya zingine nane husika marufuku hiyo imeondolewa, na shule zimetakiwa kuanza shughuli zao.
Lengo ni kuchanja watu 350,000 kwa wiki sita. Serikali inataka kuokoa muda iliyopoteza na kufikia lengo lake la 30% ya Wanyarwanda ambao watakuwa wamepewa chanjo hadi mwishoni mwa mwaka huu. Wakati mwezi Machi, Rwanda ilikuwa kati ya nchi za kwanza kuanza kampeni yake ya chanjo na kupokea dozi kutoka mpango wa kimataifa wa ugawaji chanjo kwa nchi masikini wa COVAX. Miezi sita baadaye, Warwanda 460,000 pekee, au zaidi ya 3% tu ya raia wa Rwanda, ndio wamepokea dozi mbili za chanjo.
Lakini serikali iliweza kununua dozi zaidi ya milioni tatu hivi karibuni ya chanjo ya Pfizer / BioNTech, chanzo katika Wizara ya Afya kimebaini. Dozi hizo zitatolewa hatuakwa hatua, kampeni hiyo itaanza Jumanne wiki hii huko Kigali kisha nchini kote kwa raia wenye umri wa miaka 40 na zaidi.
Wakati huo huo, viongozi wamepunguza nusu ya bei ya vipimo vya haraka vya antijeni, ambavyo vitashuka kutoka karibu euro 10 hadi 5 kwa siku chache zijazo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanzania, Elias Kwandikwa, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam
Waziri Kwandikwa, alikuwa akipata matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa karibu siku kumi na nne.
Taarifa za kufariki dunia kwa Kwandikwa zimethibitishwa na Katibu wake wa masuala ya jimboni, Julius Lugobi
Kwandikwa, mbali na kuwa Waziri, alikuwa mbunge wa Ushetu katika mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM .
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa ziarani nchini Rwanda, ametuma salamu za rambi rambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini humo, Jenerali Venance Mabeyo, Taarifa kutoka Ikulu imeeleza.
Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko kifo cha waziri huyo kutokana na mchango wake mkubwa katika utumishi wa Umma.
Kabla ya kuteuliwa katika nafasi yake ya sasa aliyokuwa akiitumikia, Kwandikwa amewahi kuhudumu katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ujenzi Masilia na Uchukizi akiwa chini ya Isack Kamwelwe.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Elysee Jumatano Mei 23. Francois Mori/Pool via Reuters
Hatimaye Balozi mpya wa Ufaransa nchini Rwanda Antoine Anfre amewasilisha barua za utambulisho kwa kiongozi wa nchi hiyo Paul Kagame.
Hatua hii inakuja baada ya Ufaransa na Rwanda kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baada ya nchi hiyo kutokuwa na Balozi wa taifa hilo la Ufaransa kufuatia madai kuwa nchi hiyo ya bara Ulaya lilishiriki kwenye mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Hivi karibuni Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alifanya ziara nchini Rwanda,z iara iiliyoangaziwa kufungua ukurasa mpya wa historia ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili.
Bwana Macron ni rais wa pili wa Ufaransa kutembelea Rwanda baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 tangu rais wa zamani Nicolas Sarkozy alipotembelea taifa hilo mnamo 2010. Rwanda ilivunja uhusiano wake na Ufaransa mwaka 2006 kwa shutuma za mauaji ya kimbari.
Rais Macron alisema ziara yake nchini Rwanda itakuwa ya « sera ya ukumbusho, uchumi na kuangazia siku zijazo. » Na kuongeza kwamba yeye pamoja na Rais Kagame walikubaliana »kuanzisha ukurasa mpya wa mahusiano na kufanya miradi ya maendeleo. »
Kiongozi wa chama cha FPI Simone Gbagbo, Agosti 11, 2020. SIA KAMBOU / AFP
Simone Gbabgo hakabiliwi tena na mashitaka kutoka Mahakama ya Kimlataifa ya Uhalifu, ICC. Waranti wa kukamatwa wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya mke wa rais wa zamani wa Côte d’Ivoire, aambaye alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa mzozo wa 2010-2011 yameondolewa.
« Mahakama inaamua kwamba hati ya kukamatwa dhidi ya Simone Gbagbo imefutwa na haina umuhimu tena, »imeandika ICC, ikijibu ombi kutoka kwa mwendesha mashtaka, katika uamuzi wa kurasa 7 wa Julai 19 na kutolewa hadharani Alhamisi jioni wiki hii.
Simone Gbagbo yuko huru kusafiri
« Habari njema kwa Bi Simone Gbagbo (…), sasa ataweza kusafiri akiwa uhuru kote ulimwenguni, » amejibu wakili wake Ange Rodrigue Dadjé, katika taarifa.
« Kuondolewa kwa waranti huu kunakuja kumaliza kabisa kesi dhidi ya Simone Gbagbo mbele ya ICC, » ameongeza.
Simone Gbagbo alikuwa ameshtakiwa na ICC tangu 2012 kwa makosa manne ya uhalifu dhidi ya binadamu, ambayo ni mauaji, ubakaji, vitendo vingine visivyo vya kibinadamu na mateso, yaliyofanywa wakati wa mzozo wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011.
Mgogoro huu, uliozuka kufuatia hatu ya Laurent Gbagbo kukataa kutambua kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais wa 2010 dhidi ya Alassane Ouattara, ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000.
Simone Gbagbo ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela
Mwezi Machi mwaka jana, ICC ilimuachilia huru Laurent Gbagbo, ambaye pia alishtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, na aliweza kurudi Côte d’Ivoire Juni 17, baada ya miaka kumi akizuiliwa Hague.
Tofauti na mumewe, Simone Gbagbo alikuwa hajawahi kukabidhiwa ICC.
Hata hivyo alihukumiwa mwezi Machi 2015 kwa miaka 20 gerezani huko Abidjan kwa kuhatarisha usalama wa taifa.
Picha za waathiriwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda katika eneo la ukumbusho la mauaji ya Kimbari huko Kigali. REUTERS/Noor Khamis
Manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda yaliyotokea mwaka 1994, wamepokea kwa furaha kurejeshwa nchini humo kutoka Uholanzi mmoja wa washukuwa wakuu Venant Rutunga ili kufunguliwa mashtaka.
Venant Rutunga, mwenye umri wa miaka 72 aliwasili mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Jumatatu jioni. Alikabidhiwa kwa maafisa wa Rwanda ambapo anatuhumiwa kuwa alikuwa sehemu ya makada ambao waliandaa mauaji ya Watutsi kusini mwa nchi hiyo.
Mnamo mwaka 1994, Venant Rutunga alikuwa mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa kilimo, Isar Rubona, karibu na mkoa wa Butare. Mauaji yalipoanza, zaidi ya wakaazi elfu moja walikimbilia katika majengo ya taasisi hiyo. Venant Rutunga anashukiwa kuleta askari na wanamgambo wa Interahamwe. Egide Nkuranga, kiongozi wa mpito wa Ibuka, shirika lisilo la kiserikali la Ufaransa linalojikita kuhusiana na kumbukumbu ya mauaji ya Watutsi nchini Rwanda, anasema hakuna shaka: Venant Rutunga alikuwa na jukumu kubwa katika utekelezaji wa mauaji ya kimbari katika sehemu hii ya nchi.
“Alikuwa miongoni mwa viongozi wa Isar. Alikuwa na nafasi kubwa, ya kutekeleza kile anacho kitaka sehemu hiyo ya nchi. Alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakifuatilia utekelezaji wa mauaji ya kimbari yaliyopangwa. Kwa hivyo, alikuwa kiongozi wa operesheni za mauaji ya kimbari ambayo yalikuwa yakitokea nch Rwanda. «
Mnamo mwaka 2000, Venant Rutunga aliomba hadhi ya ukimbizi nchini Uholanzi, lakini alikataliwa, kwa sababu ya kile anachotuhumiwa nchini Rwanda. Karibu miongo miwili baadaye, mwezi Machi 2019, kutokana na matokeo ya ushirikiano kati ya vyombo vya sheria vya Rwanda na Uholanzi, Venant Rutunga alikamatwa katika kijiji karibu na Utrecht.
Baada ya kumaliza rufaa zake zote ili kuepuka kurudishwa nchini Rwanda kuweza kuhukumiwa, anakuwa raia wa tatu wa Rwanda anayeshukiwa kwa uhalifu wa mauaji ya kimbari kurejeshwa na Uholanzi nchini Rwanda.
Kuhusu mkurugenzi mkuu wa zamani wa Isar Rubona Charles Ndereyehe, anayedaiwa kupanga mauaji ya mwaka 1994 katika eneo hili la Rwanda, alikamatwa pia Uholanzi mwezi Septemba 2020. Rwanda inasubiri kurudishwa kwake
Mwanamke akipita karibu na makao makuu ya Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) Novemba 5, 2017 huko Kinshasa. JOHN WESSELS / AFP
Viongozi wa kidini wameendelea kuvutana nchini Jamhuri ya kidemkorasia ya Congo kuhusu uteuzi wa mkuu wa tume huru ya uchaguzi CENI ambapo kuanzia mapema leo asubuhi wanatakiwa kukutana kuendelea na mazungumzo ili kupatikana kwa muafaka.
Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa kanisa Katoliki, Askofu Marcel Utembi, amewatolea wito viongozi wa kiroho kuwasili mapema hii leo katika eneo la mkutano kwa kuanza tena mazungumzo yenye lengo la kupatikana kwa muafaka juu ya uteuzi wa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, CENI.
Vikao vya shughuli hiyo vilisitishwa tangu Julai 27 baada ya viongozi wa madhehebu ya dini kushindwa kukubaliana juu ya uteuzi wa mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI).
Kanisa Katoliki lilikuwa limeamba kupewa muda zaidi.
Madhehebu sita ya kidini (Kanisa la Orthodox nchini DR Congo, Kanisa la Yesu Kristo hapa duniani kupitia mjumbe wake maalum Simon Kimbangu (EJCSK), Jumuiya ya Kiislamu nchini DRC (COMICO), Kanisa la Uamsho wa Kongo (ERC), Muungano wa Makanisa Huru ya Kongo (UEIC) na Jeshi la Wokovu) baadaye walikutana katika makao makuu ya Tume ya Uadilifu na Usuluhishi wa Uchaguzi (CIME).
Madhehebu haya ya kidini yalitangaza Julai 27 jioni kwamba walikuwa wamemteua mgombea wa jukwaa lao kuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI). Uteuzi huo ulifanywa kwa kukosekana kwa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC), ambao walisema kwamba kikao cha Jumanne kilisitishwa na kwamba kazi inapaswa kuanza tena Jumatano.
Kwa kuwa wameshindwa kufikia makubaliano juu ya mgombea mmoja, madhehebu ya kidini basi yalitafuta usuluhishi kutoka kwa spika wa Bunge la Kitaifa Christophe Mboso, ambae alikutana na pande mbili Kanisa Katoliki na lile la kiprotestanti pamoja na madhehebu sita na kuwataka kuendelea na mazungumzo ili kupatikana muafaka, na hivyo kuwapa muda wa saa 48 kumaliza tofauti zao na kutangaza jina la mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi.
Maelfu ya raia nchini Ufaransa waliandamana siku ya Jumamosi kupinga vizuizi vya kudhibiti kusambaa ugonjwa wa Covid-19 na sera za kuwalazimisha kudungwa chanjo. REUTERS – BENOIT TESSIER
Kuanzia wikendi hii na kwa muda wa wiki mbili, Visiwa vya Reunion vitakuwa chini ya masharti ya watu kutotembea mchana na sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa kuanzia saa 12 jioni hadi saa 11 Alfajiri.
Kulingana na mkuu wa mkoa, maeneo kadhaa ya mji huo yanakabiliwa na « ongezeko lisilo kuwa la kawaida ya maambukizi ya visa vya Corona ».
Hii ni mara ya kwanza tangu kutangazwa kwa hatua za watu kutotembea katika msimu wa majira ya Joto 2020. Kutokana na kuongezeka kwa kesi za Covid-19, Visiwa vya Reunion vimewekwa chini ya masharti ya watu kutotembea mchana, « kumetangzwa sheria ya kutotoka nje usiku kuanzia saa 12 jioni hadi saa 11 Alfajiri », hatua ambazo zitaanza kutekelezwa wikendi hii « kwa kipindi cha wiki mbili « , mkuu wa mkoa wa Reunion, Jacques Billant ametangaza Alhamisi jioni Julai 29.
Jacques Billant ametangaza pia kwamba mikahawa, baa na kumbi za michezo vitafungwa katika kipindi chote hicho cha wiki mbili.
Guadeloupe na Martinique zakabiliwa na ongezeko la maambukizi Hatua hizi pia zitatekelezwa katika maeneo ya Antilles ya Ufaransa kama « Gaudeloupe na Martinique » ambapo kunaripotiwa ongezeko la visa vya maambukizi. Katika maeneo haya 17% tu ya raia ndio wamepewa chanjo wakati nchini Ufaransa 50% ya raia wamechanjwa.
Ufaransa jumatano imesihi Tunisia kuteua haraka waziri mkuu mpya na serekali, wakati taifa hilo la kaskazini mwa Afrika likizidi kutumbukia kwenye hali ya kisiasa isiyokua na uhakika.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Yves Le Drian, amemwambia mwenzake wa Tunisia Othman Jerandi kwamba, wananchi wa Tunisia wanasubiri hatua kama hiyo, baada ya rais Kais Saied kufuta kazi maafisa zaidi, awali pamoja na kusitisha shughuli za bunge na kuongoza kwa amri a kiutendaji, hatua ambazo wapinzani wake wamesema ni “ mapinduzi”
Akizungumza kwa njia ya simu na Jerandi, Le Drian amesisitiza umuhimu wa uteuzi wa haraka wa waziri mkuu na kuunda serekali ambayo itaweza kukidhi mahitaji ya wananchi wa Tunisia, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa amesema.
Amesema pia kwamba kuna umuhimu wa kudumisha utulivu na sheria, na kuruhusu utendaji kazi wa haraka wa taasisi za kidemokrasia za Tunisia.
Mashirika muhimu ya kiraia ya Tunisia yameonya kuhusu kuongeza kinyume cha sheria muda wa siku 30 wa hatua ya rais Saied ya kusitisha shughuli za bunge, na yameomba katika taarifa ya pamoja, ratiba ya hatua za kisiasa.
Rais wa Burundi Evariste Ndayshimiye, wakati wa kampeni alipokuwa akigombea kiti cha uongozi wa wa chama tawala cha CNDD-FDD Gitega, Burundi, Mei 20,2020.
Serikali ya Burundi sasa inasema itakubali chanjo za COVID-19, na kuwa moja ya nchi ya mwisho ulimwenguni kupokea hiyo chanjo
Serikali ya Burundi sasa inasema itakubali chanjo za COVID-19, na kuwa moja ya nchi ya mwisho ulimwenguni kupokea. Lakini wizara ya afya nchini humo inasema haitachukua jukumu la athari yoyote ambayo inaweza kusababishwa na chanjo.
Waziri wa Afya Thaddee Ndikumana Jumatano alisema chanjo hizo zitafika kwa msaada wa Benki ya Dunia. Haikufahamika mara moja nchi hiyo itapokea dozi ngapi au lini.
Chanjo hiyo itapewa wale wanaohitaji, waziri wa afya alisema. Serikali itahifadhi chanjo lakini haitawajibika kwa athari yoyote ameongeza.
Tangazo la Burundi lilikuja siku hiyo hiyo ambayo nchi jirani ya Tanzania ilizindua kampeni yake ya chanjo, ikibadili mwelekeo kutoka kwa Rais wa zamani John Magufuli kukataa kutambua kuwepo kwa janga hilo. Alifariki mwezi Machi na urais ulikwenda kwa makamu wake Samia Suluhu Hassan, ambaye tangu wakati huo amebadili mwelekeo wa kupambana na COVID-19 katika moja ya nchi zenye watu wengi zaidi barani Afrika.
Rais wa Burundi hayati Pierre Nkurunziza, ambaye alifariki mwaka jana, pia alikosolewa kwa kudharau janga hilo. Utawala wa mrithi wake, Rais Evariste Ndayishimiye, mapema mwaka huu ulisema nchi hiyo ya watu zaidi ya milioni 11 bado haihitaji chanjo za COVID-19.
Wabunge wa somalia wainua mikoni kwenye Uchaguzi wa awali
Zoezi la kupiga kura lilianza Alhamis katika moja ya majimbo ya Somalia likiwa limechelewa kwa siku kadhaa, lakini limefanyika kabla ya nchi nzima ambapo awamu ya kwanza ya uchaguzi wa kitaifa, haijaweza hata kuanza.
Uchaguzi wa bunge na rais uliosuburiwa kwa muda mrefu ulitarajiwa kuanza tarehe 25 Julai, kulingana na ratiba ilioafikiwa na viongozi wa kisiasa baada ya miezi kadhaa ya mivutano mikali juu ya mchakato huo.
Uchaguzi nchini Somalia unafuata mfumo wakutatanisha wa uchaguzi siyo wa moja kwa moja, na katika hatua ya kwanza ya upigaji kura, majimbo matano yanatakiwa kuwachagua maseneta wa baraza la seneti katika bunge la taifa.
Lakini hakuna hata jimbo moja lililokuwa tayari, na hakuna hata jimbo moja lililopiga kura tarehe iliowekwa, na hivyo kuisambaratisha ratiba ya uchaguzi.
Jubaland, jimbo linalopakana na Kenya ambalo lilikuwa limejianda vya kutosha, lilipiga kura Alhamisi, na kuwachagua wagombea wanne kwenye baraza la seneti lenye maseneta 54.
Rais wa jimbo hilo Ahmed Madobe ameipongeza Jubaland kwa kuanzisha uchaguzi wa muda mrefu uliocheleweshwa mara kadhaa.
Ukitaja wanasoka mahiri wawili wa kizazi cha sasa duniani, jina la Cristiano Ronaldo lazima liwepo kwenye orodha hiyo, ama litakuwa la kwanza ama la pili, inategemea na tafsiri ya anayeweka orodha hiyo kati yake na Lionel Messi.
Na ukiongoeza orodha hiyo na kufikia wachezaji wane wakali waliowahi kutokea duniani, jina lake litakuwepo tu itategemea utawaorodheshaje kati yake na Messi, Edson Pele na Diego Maradona.
Hilo linakuonyesha isivyo shaka kuhusu ubira wake ndani ya uwanja akiwa na klabu yake ama timu yake ya taifa.
Amecheza Ureno kwenye Klabu ya Lisbon, Uingereza kwenye klabu ya Manchester United, Uhispania kwenye Real Madrid na sasa anakipigia Klabu ya Juventus.
Wengi hasa wafuatiliaji wa soka katika miaka ya 1990s mpaka 2000s wanamfahamu mtu anaitwa Ronaldo Luís Nazário de Lima, alikuwa maarufu kwa jina la Ronaldo, mchezaji wa zamani wa vilabu vya Inter Milan, Barcelona, Real Madrid, PSV, Corinthians na timu ya taifa ya Brazili ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara mkubwa na mmiliki wa timu ya La liga ya Real Valladolid.
Alikuwa mshambuliaji mahiri akitwaa kombe la dunia na Brazil mwaka 2002 na kutwa a tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 3. Wengi wanadhani jina la Ronaldo wa sasa limetokana na umaarufu wa Ronaldo wa zamani, la hasha Ronaldo wa sasa jina lake lina historia tofauti.
Cristiano Ronaldo Dos Santos Aveiro alizaliwa mwaka Februari 5, mwaka 1985 huko Funchal katika visiwa vya Madeira, kwa mama Maria Doroles Dos Santos Aveiro na marehemu baba yake Jose Dinis Aveiro.
Alipozaliwa tu baba yake akampatia jina la Ronaldo akimuona kama Ronald Reagan (Rais wa Marekani) ajae.
Wakati huo baba yake hakuwa na wazo kabisa kuhusu mwanae kuwa mwanasoka, alimpenda sana Rais Reagan, ambaye wakati Ronaldo anazaliwa ndio alikuwa ametoka kuapishwa kuwa rais katika awamu yake ya pili ya uongozi
Ronaldo ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watatu waliozaliwa na wazazi wake, mwingine ni Maria Dolores mwenye fani ya upishi na Jose Denis Aveiro ambaye ni askari wa zamani, mtunza bustani na mtunza vifaa. Ana ndugu wengine wakubwa kaka yake Hugo, na dada zake wawili Elma na Liliana Cátia « Katia ».
Katika utoto wake, Ronaldo alikuwa anadekezwa na kudeka kupita kiasi. Kuna wakati ndugu zake hasa kaka zake walilazimika kubeba makosa yake. Alijiliza na kujilalamisha kitoto kila alipoona amekosea, na kwa huruma zao ndugu zake wakubwa walibeba makosa yake mbele ya wazazi wao.
Baba yake José, alifariki mwaka 2005 Ronaldo akiwa na miaka 20 tu, huku mama yake akitibiwa saratani ya matiti mwaka 2007, ingawa anaendelea vyema sasa.
Wazazi wa Ronaldo walikuwa masikini wasiojiweza, ingawa walijitahidi kati ya watoto wote kumpa kila alichokitaka Ronaldo kama kitinda mimba. Ronaldo hakuwahi kukosa ngo ya aina yoyote aliyohitaji hata kama itawalazimu wazazi wake kukopa. Alipendwa sana na kila mwanafamilia kwa sababu ya uchangamfu wake na namna alivyojipenda yeye mwenyewe.
Kutokana na umasikini, mama yake alipopata mimba ya Ronaldo aliwaza kuitoa. Mama yake aliwahi kukiri kwamba umasikini, ulevi wa baba yeke na ukubwa wa familia yake iliyokuwa tayari ina watoto wengine wengi zilikuwa sababu za kutaka kutoa mimba hiyo.
Kama si daktari aliyemuhudumia wakati huo leo soka lisingekuwa na Ronaldo na lisingekuwa na mfungaji mahiri wa aina yake.
Daktari alikataa kuitoa mimba hiyo, kwa sababu za kiafya, licha ya kukubaliana naye kuhusu hali ngumu ya maisha ya familia ya Ronaldo, ambayo walilazimika watoto wote kulala katika chumba kimoja.
Baada ya daktari kukataa wazo la Maria Doroles Aveiro la kutoa mimba, mama huyo ilibidi atafute njia mbadala, akaanza kunywa pombe mpaka anakuwa hoi na kukimbia kupitia kiasi akitumaini mimba hiyo ingetoka, lakini haikuwezekana na mwishowe akaamua kuzaa tu.
Zipo tafiti na machapisho mengi yanaokinzana kuhusu historia ya Ronaldo lakini mengi yanakubaliana kwamba, nyota huyo wa kiataifa wa Ureno ana asili ya Afrika Magharibi. Kwanini wanasema hivyo? Ni kwa sababu babu yake ana asili ya Praia, Cape verde, moja ya visiwa maarufu Afrika.
Kizazi cha kwanza cha Ronaldo cha Isabel Rosa da Piedade(babu na bibi zake) walizaliwa na kuishi Praia, kizazi kilichofuata cha Cirilo Aveiro ambaye ni babu wa baba yeke kikiwa na miaka 16 walikimbilia kisiwa cha Medeira, na hapo vikafuata vizazi vitatu mpaka cha Ronaldo.
Kwa sababu ya asili hiyo, waafrika hasa wa Cape Verde wanamuona ni ndugu yao wa damu, licha ya kuwa na uraia wa ureno kutokana na kuzaliwa kwa baba na babu waliokuwa na uraia wa nchi hiyo.
Ronaldo alianza kuonyesha kupenda soka toka akiwa na umri mdogo kabisa, na baba yake alianza kuona hilo na kuanza kumpeleka viwanjani. Licha ya kuanza shule lakini hakuwa na mpango na shule na mara kadhaa aliacha masomo na kumsindikiza baba yake kwenye klabu ya Andorihna huko Funchal, aliyekuwa mtunza vifaa wa timu. Alipotimiza miaka 8 akasainiwa timu ya watoto ya klabu hiyo.
Katika kumsaidia zaidi, baba yake Jose Aveiro akaamua kuacha kazi katika timu ya wakubwa na kuwa mtunza vifaa wa timu ya watoto, ili kuwa karibu na mwanae na kumsaidia kukua katika soka.
Mchezaji mwenzake wa Andorinha wakati huo wakiwa wadogo, ambaye kwa sasa ni kocha akionoa mpaka Andorihna yenyewe, Ricardo Santos, aliwahi kunukuliwa akisemema ‘C. Ronaldo alikuwa anapenda kushinda, ikitokea timu imefungwa, analia sana, alikuwa analia sana mpaka akapachikwa jina la mtoto mlizi’,.
Akiwa na miaka 12 , akaondoka Medeira na kwenda Lisbon kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kisoka akiwaacha wazazi wake. Akafanya mjaribio ya siku 3 katika timu ya watoto ya Sporting Lisbon na kufaulu na kusajiliwa kwa Pauni 1,500 tu ilikuwa mwaka 1997.
Upweke katika jiji la Lisbon ulimliza kila leo ‘mtoto mlizi’, lakini alijiambia anapaswa kupambana kusaidia kuondoa umasikini wa wazazi wake
Matatizo ya Moyo na tishio la kuacha soka
Akiwa Sporting Lisbon, alianza kuonyesha dalili za kuwa na matatizo ya moyo. Hakuwa sawa, na kuna wakati moyo wake ulionekana kushindwa kufanya kazi sawa sawa. Madakatari wa Klabu hiyo ilibidi waombe ruhusa kwa wazazi wake ili kumfanyia upasuaji, kwa sababu bila kufanya hivyo soka angelisikia kwenye redio.
Damu ilikuwa haitembei vizuri mwilini kwa msukumo wa moyo uliokuwa na shida. Wazazi wake walifarijika na hilo, matibabu yalifanyika na kufanikiwa kurejea uwanjani.
Ronaldo alikuwa mchezaji muhimu katika timu ya vijana ya Sporting Lisbon ya Ureno, lakini safari yake ilianza vyema baada ya kocha wa timu ya wakubwa, Laszlo Boloni kumpa nafasi wakati wa mechi za kujiandaa na msimu. Na katika moja ya mechi za kirafiki kati ya timu hiyo na Manchester United, iliyopigwa Agosti 6, 2003 akiwa na miaka chini ya 18, Ronaldo alicheza soka la uhakika pamoja na umri wake mdogo na kuwafanya wachezaji wakongwe wa Manchester wakati huo kumuomba kocha Sir Alex Ferguson kumsajili haraka.
‘Tulikuwa kwenye basi tunamsubiri mtendaji mkuu David Gill na meneja Ferguson, tulisukuma asainiwe, na ndani ya wiki moja alikuwa mchezaji wa Manchester United’, alisema Rio Ferdinand, beki wa zamani wa Manchester.
‘Kila kitu kilienda haraka sana, siku mbli baadae nilizungumza na kocha wakanipokea England, Manchester nikasajiliwa’, alisema Ronaldo kwenye moja ya mahojiano yake.
Beki mwingine Mikael Silvester aliwahi kunukuliwa akisema ; alicheza kwa kiwango cha juu siku hiyo, kabla ya mchezo kuanza hakuna aliyekuwa anamjua, lakini baada ya mchezo kila mtu alimjua’, alisema kuhusu mechi hiyo ambayo Manchester ililala kwa mabao 3-1.
Licha ya kwamba alishafanya mazungumzo na Arsen Wenger kwa ajili ya kujiunga na Arsenal, Manchester walimsajili haraka na kwenda kuwa mchezaji mkubwa duniani. Katika miaka 6 aliyokuwa Manchester alishinda mataji matatu ya ligi kuu na moja la klabu bingwa Ulaya huku akiifungia mabao 118.
Akaenda Real Madrid kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa pauni 80mil, akiwa pale akashinda karibu kila kitu kitu ikiwemo mataji mawili ya la liga na manne ya ligi ya mabingwa Ulaya, kabla ya kutimikia Juventus mwaka 2018 ambapo ameshinda mataji kadhaa yakiwemo mawili ya Seria A.
Ukiacha makombe lukuki aliyoyazoa akiwa na vilabu vya Manchester United, Real Madrid na sasa Juventus, Ronaldo ana tuzo binafsi zaidi ya 40 kutokana na mchango wake kwenye timu alizowahi kuchezea, ikiwemo tuzo ya mwanasoka bora wa dunia ‘Ballon dor aliyotwaa mara tano , mara moja nyuma ya Lionel Messi.
ByAmekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake ya taifa ya Ureno, ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo kwa mabao yake 109 akiipa pia taji la Euro mwaka 2016. Mbayo yake matano katika michuano ya Euro 2020 yamemfanya kufikisha mabao 109 akiwa na timu ya taifa 109 na umfikia Ali Daei wa Iran aliyekuwa mchezaji mwenye magoli mengi zaidi ya timu ya taifa duniani.
Ronaldo pia ndiye mfungaji bora wa muda wote wa michuano ya Ulaya akiwa na mabao 14 akimpiku Michel Platin mwenye mabao 9 na Antoine Griezmann mwenye 7.
Mafanikio makubwa aliyapata zaidi akiwa na klabu yake ya Real Madridi alipoipachikia mabao 450 katika michezo 438. Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza anayeendelea kucheza kuingiza zaidi ya dola $bilioni 1 katika maisha yake ya soka huku mkataba wake wa miaka minne na Juventus unaomalizika mwaka 2022 ukimuingizia wastani wa $64milioni.
Ronaldo si mtu wa kujikweza sana, lakini mtindo wake wa maisha unamtofautisha kiasi na mastaa wengine duniani. Ana wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii, akifikisha wafuasi 500milioni kwenye mitandao ya Facebook, Instagram na Twitter.
Hana Tatoo mwilini mwake kama watu wengine maarufu na amekuwa akipenda sana kuchangia damu. Pia Si mtu wa starehe za pombe ama kwenda kwenye majumba ya starehe sana, lakini amekuwa na mahusiano mengi, mtaani unaweza kumwita ni mtu wa ‘totoz’.
Ronaldo ana watoto wanne, wa kwanza ni Cristiano Jr. aliyezaliwa Juni 17 2010 huko Marekani kwa mama ambaye, amefichwa utambulisho wake kwa mkataba.
Januari 2015, Ronaldo alieleza umma uhusiano wake wa miaka mitano na mwaamitindo wa Urusi Irina Shayk ulikoma. Kwa sasa ana uhusiano na mrembo mwingine wa Hispania Georgina Rodríguez, muuza duka msaidizi wa zamani ambaye wamefanikiwa kuzaa binti yake wa mwisho Alana Martina, aliyezaliwa Novemba 12 2017.
Ingawa ana mapacha wengine, mmoja wa kike mmoja wa kiume, Ronaldo amekuwa mwingi wa habari kwa mabinti, akiwa na mahusiano na mabinti mabalimbali ambao wengi wao ni warembo na wanamintindo.
Inatajwa mpaka mwaka huu, amewahi kuwa na uhusiano na mabinti 31 tofauti tofauti katika maisha yake, ambao wengi kati yao wanafahamika na maarufu, ingawa wapo ambao hawafahamiki na pengine yeye kutowafahamu kwa majina.
Baadhi ya wapenzi wake ni Merche Romero, Nereida Gallardo, Kim Kardashian, Irina Shayk, Rita Pereira, Andressa Urach na Georgina Rodriguez.
Inaelezwa kuwa uhusiano wa kukutana na mtu kwa ahadi ya kufanya tendo la ndoa tu na kuachana kila mtu kivyake, umemuingiza katika makubaliano ya siri. Mtoto wake wa kwanza Ronaldo Jr, mama yake ambaye hajulikani, ameingia mkataba na Ronaldo wa kutojitambulisha kuhusu mtoto huyo na kukaa naye mbali. Mtoto huyo kalelewa na bibi yake ambaye ni mama yake na Ronaldo.
Urafiki wawawili hawa ulijulikana kwenye moja ya matukio ya Ronaldo kupokea tuzo aliposema ‘ Kweli mimi ni mchezaji bora na mafanikio haya yote ni kwa sababu ya moyo mzuri wa rafiki yangu akimuonyeshea Fantrau.
Ronaldo aliendelea kusema ‘ tulikuwa tunacheza pamoja timu ya watoto mtaani, walipokuja wasaka vipaji wa Sporting Lisbon kutuangalia walitueleza, mshambuliaji atakayefunga mabao mengi atakwenda Spots Academy, ambayo ni hatua muhimu ya kuelekea timu ya wakubwa na kukua kisoka. Siku hiyo tulishinda mabao 3-0. Nilifunga goli la kwanza, Alberto akafunga la pili, lakini goli la tatu ndilo lililoleta mvuto zaidi. Alberto alibaki yeye na kipa tu akampiga chenga kipa kilichobaki ilikua kufunga goli lililokuwa wazi. Wakati huo nilikuwa nakimbia upande wake, sasa badala ya kupiga na kufunga akanipasia mie nikafunga, na hiyo ndio sababu nipo hapa leo’.
Lakini baada ya mechi kumalizika nilimuuliza ‘Kwanini ulifanya vile? Akajibu ‘ kwa sababu najua kwamba wewe ni mchezaji mzuri kuliko mie na utafika mbali kwenye soka, ulihitaji kupewa msaada ule’,
Mpaka leo watu hawa ni mrafiki wa kutupwa, wasioachana licha ya mara kadhaa kutengenishwa na majukumu yao.
Mafanikio yake na tuzo alizotwaa yamemfanya kuanzisha jumba la kumbukumbu lililoko huko alikozaliwa Funchal Madeira linalosimamiwa na kaka yake. Juu ya jumba hilo la makumbusho kuna hotel yake maarufu aliyoianzisha kwa kushirikana na Pestana Group.
Nje ya jumba hilo kuna sanamu lake na nembo kubwa ya CR7, C ikisimama kwa jina lake Cristiano, R ni Ronaldo na 7 ni namba ya jezi iliyompa umaarufu akiwa na Manchester United na Ureno.
Mbali na historia ya gwiji hili utakayoipata kwenye jumba hilo, pia tuzo na makombe yote 126 aliyoshinda binafsi na timuzake utayapata. Limepambwa na nakshi za picha zake, akiwa na jezi za timu mbalimbali alizochezea. Jumba hili la makumbusho lenye ukubwa wa mita za mraba 400 alikuwa analisimamia kaka yake, Hugo Dinarte Aveiro.
Wanajeshi wa DRC katika Kijiji Cha manzalao karibu na Beni Feburi 2020 (picha ya zamani
Wanajeshi sita, ikiwa ni pamoja na maafisa waandamizi wa jeshi la DRC walioko Beni, mashariki mwa nchi hiyo wako chini ya sheria ya mahakama ya kijeshi tangu Jumanne (Julai 27).
Kulingana na msemaji wa Ukaguzi Mkuu wa jeshi la FARDC, wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa pesa zilizokusudiwa wanajeshi waliopelekwa mashariki mwa DRC kama sehemu ya mapambano dhidi ya makundi yenye silaha.
Hii ni sehemu ya operesheni ya ukaguzi uliozinduliwa zaidi ya wiki moja iliyopita, na ambayo inahusu mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini, iliyowekwa chini ya amri ya kijeshi. Kabla yao, maafisa wengine 11 walikamatwa huko Bunia.
Kanali Polydor Lumbu Mutindu anayehusika na maswala ya utawala katika Sekta ya utendaji ya Sukola 1 Grand Nord na maafisa wanne ni miongoni mwa maafisa hao wa jeshi waliowekwa chini ya sheria ya mahakama ya kijeshi.
Majina ya majenerali
Kulingana na msemaji wa Ukaguzi Mkuu wa Jeshi, wote wanahusika katika ubadhirifu uliothibitishwa. Maafisa hawa watakabidhiwa kwa mkaguzi mkuu huko Goma kwa. Hata hivyo operesheni hiyo bado inaendelea.
Ukaguzi Mkuu wa Jeshi umeahidi kuweka wazi kila kitu ifikapo Jumamosi, wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Majina ya baadhi ya majenerali, ambao wanakabiliwa na mashaka makubwa ya ubadhirifu, yatatangazwa.
Askari wa jeshi la Drc katika Kijiji karibu na beni ( kivu ya kasikazini) febuari 18,2020 (picha ya kmbukumbu)
Watu wanane akiwemo mwanajeshi wa serikali, wameuawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea hivi punde katika maeneo ya Bulongo, umbali wa Kilomita 30 kutoka mjini Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Miongoni mwa manusura ni mtoto wa umri wa miezi Sita aliye kutwa pembezoni mwa maiti ya mama yake.
« Rafiki yangu mwenye tulikuwa naye shambani amechinjwa, mimi Mungu Alinisaidia nilipigwa risasi nikaangukia bondeni ,wahalifu walikuwa wanaongea lugha ya Kiswahili, huku wakivamlia sare yenye mstari mweupe, » amesema mmoja wa manusura.
Mbunge wa kitaifa Paul Vahumawa amehuzunishwa na kitendo hicho na kusikitishwa na kutotiliwa maanani taarifa zinazo tolewa na raia.
Bulongo ni mji ambao una vituo vingi vya askari, tulikubaliana mji huo na maeneo jirani kuwa chini ya amri za kijeshi ili hali kama hii ikomeshwe , tunaomba kabla ya kuongezwa muda kwa utawala wa kijeshi yachunguzwe yaliyofanywa hadi sasa.
Liwali wa Mkoa wa Kivu kaskazini Constat Ndima amewatolewa wito raai kuwa na subira.
Huyu adui hana ngome, angekuwa na kambi jambo hilo tungekuwa tumelimaliza mapema , tunalala na kutembea pamoja na adui , mitaani msituni, mashambani watu wanauawa , ni vigmu kwa jeshi la taifa kukabiliana na uhalifu huu kwani wanoutekeleza wanajifananisha na raia wa kawaida. Na jambo lingine ambalo tusisahu kumtafuta kote misituni wilayani Beni, sio kazi rahisi , lakini kwa ushirikiano na raia tunaweza kufikia malengo.
Wiki hii raia wengine sita waliuawa katika maeneo ya Irumu na Beni, huku magari matatu yakichomwa moto , Jeshi limedai kuwaua waasi 15 na kupoteza askari wake 7.
Raïs wa Umarekani Joe Biden kwenye picha ya maktaba
Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden umezindua program inayolenga kufanya biashara na mataifa ya kiafrika kwa jina Prosper Africa Build Together, wakati ukiomba dola milioni 80 kutoka kwa bunge ili kufaulisha mradi huo.
Baadhi ya wataalam wanasema kuwa ushirikiano wa kifedha kati ya Marekani na Afrika utaimarisha uhusiano wa bara hilo na Marekani.
Wakati akizungumza kwa njia ya kimitandao Jumatano, mratibu mkuu wa Marekani kwenye masuala ya Afrika akiwa mbele ya baraza la kitaifa la usalama, Dana Banks alisema kuwa Marekani iko tayari kufanya biashara na Afrika.
Program ya Prosper Africa inalenga kuongeza viwango vya biashara kati ya Marekani na Afrika. Hii siyo mara ya kwanza kwa Marekani kubuni mpango kama huo. Mwaka wa 2000, rais Bill Clinton alitia saini mkataba wa AGOA ambao ulitoa nafasi kwa mataifa ya kiafrika kuleta bidhaa za aina 6,500 tofauti hapa Marekani bila kulipia ushuru. Mpango huo bado unaendelea baada ya kuongezwa muda wake hadi 2025.
Kulingana na taasisi ya kiuchumi ya Brookings, Afrika kusini mwaka wa 2019 ilijipatia dola milioni 917 kutokana na mauzo ya magari na vifaa vya kilimo Marekani.
Utafiti tofauti uliyofanywa na chuo kikuu cha Afrika kusini mwaka wa 2017 unaonyesha kwamba Marekani iliagiza asilimia 10 ya mvinyo wake kutoka Afrika kusini kwa gharama ya dola milioni 59.
Sasa hivi Marekani iko kwenye mazungumzo ya kibiashara na Kenya, wakati Banks akisema kuwa Marekani ina ari ya kushiriki kwenye ukuaji wa kiuchumi wa Afrika.
//Banks Act 2//
Kupenya kwa Afrika kwenye soko la kimataifa pamoja na utamaduni ulioibuka wa kibiashara vinatoa nafasi kwetu ya kuimarisha uhusiano wetu ili kuimarisha uchumi pamoja na kutoa nafasi za ajira kwa watu barani humo.//
Gerrishon Ikiara, ni mhadhiri wa masuala ya kiuchumi kutoka chuo kikuu cha Nairobi na anasema kuwa mpango huo utaimarisha uhusiano kati ya Marekani na Afrika.
Anasema kuwa lengo la Marekani ni kuimarisha uhusiano wa kiuchumi pamoja na kisiasa kwa kutumia umaarufu wake wa kimataifa. Anasema pia Marekani katika siku za karibuni imetambua bidhaa kutoka Afrika kutokana na wahamiaji wengi kutoka barani humo wanaofanya kazi Marekani.
Hata hivyo baadhi ya wakosoaji wanasema kwamba hatua hiyo huenda ijahujumu soko huro kati ya mataifa ya kiafrika ambalo lilibuniwa mwaka wa 2019 kwa lengo la kuruhusu usafirishaji huru wa bidhaa na watu kati ya mataifa.
Waziri wa Umarekani Antony Blinken akiwa ziarani India
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken leo atakutana na viongozi wa India akiwa katika ziara yake ya kwanza nchini humo kama mwanadiplomasia wa ngazi ya juu. Maafisa wa India wanatarajia kuzungumzia wasiwasi wao juu ya kujiimarisha kwa wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Afghanistan pamoja na kuishinikiza Marekani kuiunga mkono zaidi India dhidi ya China. Kwa upande wake waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani anatarajiwa kuzungumzia wasiwasi uliopo juu ya haki za binadamu wakati atakapokutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi na waziri mwenzake wa mambo ya nje Subrahmanyam Jaishankar.Uhusiano wa Marekani na India kihistoria umekuwa wa misukosuko lakini suala la China kuzidi kujiingiza katika mgogoro na India kumeifanya Marekani na India kuwa karibu na hasa tangu mapigano makali yaliyosababisha umwagikaji damu mwaka jana katika mgogoro wa eneo la mpaka baina ya India na China la Himalaya. India ni sehemu ya ushirikiano na Marekani,Japan na Australia dhidi ya China.Ingawa kuna hisia kwamba uungaji mkono wa Marekani kwa India chini ya utawala wa rais Joe Biden sio mkubwa kama ilivyokuwa chini ya Donald Trump ambaye maafisa wake waliikosoa waziwazi China na kuiunga mkono India katika mgogoro wake na China.
Tanzania leo inazindua zoezi lake la utoaji chanjo ya Corona katika hafla ambayo rais Samia Suluhu anatarajiwa kuchanjwa katika Ikulu ya Dar es Salaam.
Serikali kupitia wizara ya Afya nchini humo imesema dozi za chanjo zitapelekwa katika kila mkoa wa taifa hilo ili kuhakikisha kwambawatu wanachanjwa.
Mkurugenzi wa Kinga Leonard Subi amesema wameamua kupeleka chanjo katika kila mkoa ili kutowabagua wanaotaka kuchanjwa kinyume na mpango wa hapo awali wa kuipeleka chanjo katika mikoakumi mikubwa .
Chanjo hiyo itatolewa kwa usawa kulingana na idadi ya watu na mahitaji yake Waziri wa Afya Dorothy Gwajima amesema jana kwamba chanjo zitakazotumiwa pole pole katika maeneo mengine zitahamishwa hadi katika sehemu zinazowachanja watu kwa haraka .
Bi.Gwajima amesema mpango wa chanjo utawalenga watu katika makundi ya vipaumbele kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.
Aliongeza kwamba chanjo nyingine zinatarajiwa nchini wanapoendelea kuzitumia zaidi ya dozi milioni moja zilizongia Tanzania mwisho mwa wiki kupitia mpango wa Covax.
Samia amewaongoza maafisa wengine wa serikali wakiwemo Waziri mkuu Kassim Majaaliwa kupokea chanjo hiyo .
Katika uzinduzi wa hafla ya chanjo chini humo rais Samia amesema serikali yake itahakikisha kwamba kila mtanzania nayetaka kuchanjwa anapata chanjo hiyo .
‘Mimi ni mama ya watoto wanne,mimi ni bibi wa wajukuu kadhaa na pia mimi ni mke ..siwezi kujiweka katika hatari … Nimekubali kwa hiyari yangu na najua ndani ya mwili wangu nina chanjo kadhaa na nimeishi nazo kwa miaka karibu 61’ alisema rais Samia kabla ya kuchanjwa.
Katika hotba yake wakati wa uzinduzi huo rais Samia aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo akisema kuna walioathiriwa na kuwapoteza jamaa zao ambao wangefurahia kuipata chanjo hiyo mapema .
‘ Wakati gonjwa hili linapokuguza ndipo utajua hatari yake…nenda Moshi,nenda Kagera ,nenda Arusha..wana maneno ya kukuambia’ alisema rais Samia .
Rais Samia alisema kuna Watanzania ambao tayari walishachanjwa nje ya nchi ili kuendelea na shughuli zao za kibiashara na kikazi .
‘Tunajua watu ambao wameshanjwa.Wameeda kuchanja Afrika Kusini au Dubai ..na wanajua kama hawangechanjwa wangezuilika kufanya biashara huko’
Aliongeza kuwa kuna makundi ya watu ndani ya nchi hiyo waliotaka kuruhusiwa kuleta chanjo hapo awali .
Jumuiya ya Wachina ilitaka kukubaliwa kuleta chanjo yao lakini serikali wakati huo ilikataa ila baadaye walikubaliwa na wamechanja .
Samia pia aliongeza kwamba wafanyikazi wa taasisi za kimataifa pia sasa wameruhusiswa kuleta chanjo na wanaendelea kuchanjwa .
Dozi Zaidi
Rais Samia amesema Tanzania imeagiza dozi zaidi za chanjo ya Johnson and Johnson kupitia Umoja wa Afrika kama alivyoshauriwa na mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika (Africa CDC) Dkt. John Nkengasong, wakati alipofanya mazungumzo naye siku ya jumanne .
‘Kwa walio tayari kuchanjwa tutahakikisha wanaipata ..chanjo ni imani . Mimi nimechanjwa mara tano au sita,’ alisema rais Samia
Chanjo katika Mikoa
Serikali kupitia wizara ya Afya nchini humo imesema dozi za chanjo zitapelekwa katika kila mkoa wa taifa hilo ili kuhakikisha kwambawatu wanachanjwa.
Mkurugenzi wa Kinga Leonard Subi amesema wameamua kupeleka chanjo katika kila mkoa ili kutowabagua wanaotaka kuchanjwa kinyume na mpango wa hapo awali wa kuipeleka chanjo katika mikoakumi mikubwa.
Chanjo hiyo itatolewa kwa usawa kulingana na idadi ya watu na mahitaji yake Waziri wa Afya Dorothy Gwajima amesema jana kwamba chanjo zitakazotumiwa pole pole katika maeneo mengine zitahamishwa hadi katika sehemu zinazowachanja watu kwa haraka.
Bi.Gwajima amesema mpango wa chanjo utawalenga watu katika makundi ya vipaumbele kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.
Aliongeza kwamba chanjo nyingine zinatarajiwa nchini wanapoendelea kuzitumia zaidi ya dozi milioni moja zilizongia Tanzania mwisho mwa wiki kupitia mpango wa Covax.
Mmoja wa afisa wa Polisi aliyekuwa analinda eneo la Capitol Hill jijini Washington DC nchini Marekani, makao makuu ya bunge amesema alihofia huenda angeuliwa na waandamanaji waliokuwa wanamuunga mkono rais wa zamani Donald Trump
Maandamano hayo yalishuhudiwa Januari 6 wakati waandamanaji hao walipovamia majengo ya bunge kudai wizi wa kura.
Afisa huyo Aquilino Gonell ameilezea Kamati ya Congress inayochunguza maandamano na vurugu hizo hali ilivyokuwa.
Waandamanaji zaidi ya 500 walikamatwa na kusababisha vifo vya watu watano, akiwemo afisa mmoja wa polisi.
Rais wa Marekani Joe Biden katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya maafisa wa Idara ya ujasusi huko McLean, Virginia, Julai 27, 2021. AP – Susan Walsh
Rais wa Marekani Joe Biden ameikosoa Urusi kwa kutaka kuvuruga uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani uliopangwa kufanyika 2022 kwa kueneza « habari mbaya ». Taarifa iliyotangulia mkutano Jumatano hii, Julai 28 kati ya Manaibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na Marekani, zaidi ya mwezi mmoja baada ya mkutano wa Geneva kati ya Joe Biden na Vladimir Putin.
« Angalia kile Urusi imefanya kuhusiana na uchaguzi wa 2022 na habari mbaya. Ni ukiukaji dhahiri wa uhuru wa nchi yetu! Joe Biden hakutaka kupitisha upande maneno yake wakati alipozuru Ofisi ya kitaifa idara ya Upelelezi karibu na mji wa Washington, akimaanisha habari anayopokea juu ya suala hili wakati wa mkutano wa kila siku.
Katika msimu wa 2022, kutafanyika uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani, ambapo viti vyote katika Baraza la Wawakilishi na theluthi moja ya viti katika Bunge la Seneti vinapitiwa upya.
Rais wa Marekani pia alimshambulia mwenzake wa Urusi Vladimir Poutine: rais wa Urusi « ana tatizo kweli keli, yeye ndiye kiongozi wa nchi yenye uchumi ambayo ina silaha za nyuklia na visima vya mafuta na sio kitu kingine chochote. Hiyo inamfanya awe hatari zaidi kwa maoni yangu
Karibu wahamiaji 60 wamefariki duni katika pwani ya Libya wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania ili kuingia Ulaya, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM.
Karibu wahamiaji 60, wakiwemo wanawake na watoto, wamifariki dinia baada ya boti lao kuzama Jumatatu wiki hii katika paniya Libya, mkasa mpya wa wahamiaji haramu katika Bahari ya Mediterania, liliripoti Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
« Wahamiaji wasiopungua 57 walikufa maji katika ajali ya boti katika iliyotokea kwenye mji wa Khoms Jumatatu hii, » IOM ilisema. Jiji la Khoms linapatikana kilomita 120 kutoka mji mkuu Tripoli katika pwani ya magharibi ya Libya, nchi ya Afrika Kaskazini ambayo ilitumbukia katika machafuko tangu mwaka 2011.
« Manusura ambao walizungumza na wafanyakazi wetu walisema wanawake 20 na watoto wawili ni miongoni mwa waliopoteza maisha, « IOM imeongeza kwenye akaunti yake ya Twitter.
IOM haijatabainisha uraia wa wahamiaji hao, lakini picha zilizotolewa na shirika hilo zinaonyesha wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada wakitoa chakula na maji kwa manusura walioonekana wamechoka, wote wakionekana kutoka nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Libya ni sehemu muhimu ya kupitia kwa maelfu ya wahamiaji wanaotafuta kila mwaka kuingia Ulaya kupitia pwani za Italia, umbali wa kilomita 300 kutoka Libya. Idadi ya wahamiaji waliokufa baharini wakijaribu kuingia Ulaya imeongezeka zaidi ya mara mbili mwaka huu, IOM ilisema katikati ya mwezi Julai. Karibu watu 900 wamekufa maji katika Bahari ya Mediterania mwaka huu.
Denis kadima, mukurugenzi mtandaji wa tasisi wa uchaguzi kuusu Demokrasia endelevu Afrika, na mgombeya kwenye kiti Cha mkuu wa CENI kutoka kanisa la kimbanguist, uko kinshasa
Viongozi wa dini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameshindwa kuja na jina moja la Mwenyeketi mpya wa Tume ya Uchaguzi nchini humo CENI, baada ya mazungumzo ya siku kadhaa.
Siku ya Jumanne, viongozi wanane wa dini kutoka madhehebu ya Kikiristo na dini ya Kiislamu walikutana kwenye makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, lakini wakashindwa kuafikiana kuhusu ni nani aongoze Tume hiyo.
Mvutano ulianza pale, viongozi wa Kanisa Katolilki na Kiprotestanti walipoomba muda zaidi wa kupitiwa kwa majina ya baadhi ya wagombea, kinyume na mtazamo wa vongozi wa madhehebu mengine sita.
Hata hivyo, viongozi hao wa dini hawakueleza kwa kina kuhusu tofauti zao huku wakisisitiza kuwa, wako pamoja na watawasilisha ripoti ya mwisho bungeni siku ya Jumatano.
Mpaka sasa, hakuna jina rasmi lililotajwa lakini duru zinasema kuwa viongozi wengi wamependekeza jina la Denis Kadima, ambaye viongozi wa Kanisa Katoliki na Makanisa ya Kiprotestanti wanaomwona mshirika wa karibu wa rais Felix Tshisekedi
Raïs wa ivory coast Alassane Ouattara akiwa na Laurent Bagbo jamanne mjini Abidjan
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara Jumanne amekutana na hasimu wake wa kisiasa wa muda mrefu, ambaye ni rais wa zamani wa taifa hilo Laurent Gbagbo, huku wakikumbatiana, ikionekana ni hatua kubwa katika kutuliza taharuki za kisiasa kwenye taifa hilo la Afrika magharibi.
Shirika la habari la Reuters limesema kuwa Ouattara alianza kwa kumwambia Gbagbo kwamba amefurahi kumuona wakati wakikutana kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha muongo mmoja kwenye makao ya rais mjini Abidjan.
Wawili hao kwanza walikumbatiana kabla ya kuvua barakoa zao na kisha kutabasamu mbele ya kamera. Kwa zaidi ya muongo mmoja, Ivory Coast ambayo ni mzalishaji mkubwa wa cocoa imekumbwa na migogoro ya kisiasa na ghasia.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 2010 hadi 2011 viliuwa zaidi ya watu 3,000 wakati viongozi hao wawili walipokuwa wakigombea utawala wa taifa hilo. Ghasia hizo zilizuka baada ya Gbagbo aliyekuwa rais kukataa kukubali kushindwa na Ouattarra kwenye uchaguzi wa Decemba 2010.
Baada ya mapigano hayo alikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uhalifu wa kivita mbele ya mahakama ya kimataifa ya jinai ya ICC, lakini mashtaka yalifutwa mwaka 2019. Gbagbo amesema katika mkutano wao alimsihi Ouattara kuendelea na juhudi za maridhiano pamoja na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa waliozuiliwa.
Ingawa serikali ya Ouattara iliruhusu Gbagbo kurejea nyumbani mwaka huu, bado anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 alichopewa Novemba 2019,wakati akiwa uhamishoni kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za benki kuu. Kufikia sasa serikali haijasema iwapo inapanga kumchukulia hatua au amesamehewa
Wiki iliopita, Tanzania ilipokeya dozi zaidi ya miliobi Moja ya chanjo ya Johnson & Johnson kutoka Umarekani kupitia mfumo wa covax
Wizara ya afya nchini Tanzania, imetangaza masharti mapya yanayolenga kusaidia kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.
Watu nchini humo wametakiwa kuvaa barakoa kila wakati na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, ikiwa ni pamoja na wito wa kuahirishwa kwa sherehe za harusi, huku mikusanyiko ya watu kwenye majumba ya Ibada ikitakiwa kupungua.
Wiki iliyopita, Tanzania ilipokea dozi zaidi ya Milioni moja ya chanjo ya Johnson & Johnson kutoka Marekani kupitia mfumo wa Covax.
Marekani imesema kwamba hatua hiyo ni miongoni mwa mpango wa kusambaza dozi milioni 25 za chanjo katika mataifa ya Afrika.
Chanjo hizo zitatumika na mahujaji, wafanyakazi wa afya, wale wa huduma za hoteli, wafanyakazi wa balozi na wagonjwa wa corona.
Wakazi wa somalia wakusanyika kutokana na mgogororo kati ya serikali na upinzani katika siku za nyuma
Uchaguzi wa Somali wa wabunge usiyo wa moja kwa moja uliyotarajiwa kuanza Jumapili umecheleweshwa kwa mara ya pili kutokana na kuwa mabunge ya majimbo kutokuwa tayari.
Kuna hofu kwamba kucheleshwa zaidi kwa zoezi hilo huenda kukahatarisha uthabiti wa kisiasa wa taifa hilo. Kufikia Jumatatu, hakuna tarehe mpya ya uchaguzi wa bunge iliyo tangazwa baada ya kuahirishwa Jumapili.
Kamati ya serikali kuu inayosimamia uchaguzi huo imesema kuwa zoezi hilo lilicheleweshwa baada ya viongozi wa majimbo matano kuchelewa kuwasilisha orodha ya mwisho ya wagombea. Kamati hiyo pia imesema kuwa hakukubuniwa kamati za kieneo za kusimamia uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya uchaguzi Mohamed Hassan Irro amesema mikakati ya kuendelea na zoezi hilo bado ipo licha ya kucheleweshwa.
Uchaguzi wa rais na bunge wa Somalia ulikuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa muhula wa rais Mohamed Abdullahi Farmajo mwezi Februari , lakini migogoro kati ya serikali na upinzani ikasababisha kucheleweshwa kwa miezi kadhaa.
Upinzani hata hivyo unasema kuwa unatarajia kuwa zoezi hilo litaendelea bila matatizo katika wiki zijazo licha ya kucheleweshwa kulingana na Mohamed Hassan Idris ambaye ni mbunge kutoka upinzani na ambaye anagombea tena katika jimbo la Jubbaland.
Zaidi ya wagombea 15 tayari wametangaza nia ya kugombea urais dhidi ya Farmajo kwenye uchaguzi uliyopangwa kufanyika Oktoba 10, na ambao utapigiwa kura na wabunge 329 .
Katika taarifa nyingine ni kwamba kundi la kigaidi la al Shabab linalofanyia opereseheni zake nchini humo, na lililovuruga uchaguzi wa 2017, limeonya wajumbe kutoshiriki kwenye uchaguzi wa ubunge na urais mwaka huu.
Taarifa hiyo iliotolewa wiki iliopita ilisema kwamba chanjo hiyo itaanza kupatiwa watu walio hatarini kukabiliwa na maambukizi, wafanyakazi wa afya, mahujaji , wafanyakazi muhimuna wasafiri wa mara kwa mara huku chanjo nyengine zikitarajiwa mwezi Disemba mwaka huu.
Hatahivyo kuanzia tarehe sita mwezi Julai 2021 kulingana na chombo cha habari cha The Citizen, kisiwa cha Zanzibar tayari kilikuwa kimeanza kutoa dozi ya chanjo hiyo kwa wafanyakazi wa Afya na wale walio katika hatari ya maambukizi.
Kulingana na wizara ya afya kiswani humo chanjo iliokuwa ikipewa wafanyakazi hao wa Afya ilikuwa ikifadhiliwa na serikali ya Zanzibar.
Taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa katika harakati ya kujiunga na mipango ya Corona barani Afrika tangu kifo cha aliyekuwa kiongozi wake John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akipinga uwepo wa ugonjwa huo na tiba ya chanjo.
Hatahivyo tangu alipochukua mamlaka rais mpya Samia Suluhu Hassan ameonesha ishara kwamba amekuwa akiupa kipau mbele ugonjwa huo.
Taifa hilo ni miongoni mwa mataifa manne ya Afrika ambayo hayajaaanzisha mpango wa kitaifa kutoa chanjo kwa raia, kulingana na Kituo cha udhibiti na uzuiaji wa magonjwa Africa ACDC.
Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi wawahi katika vituo vya huduma za afya mara waonapo dalili za mafua makali, maumivu ya koo, kichwa kuuma, kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula na kupoteza uwezo wa kunusa harufu mbalimbali.” Amesema chanjo hiyo ipo tayari nchini mwananchi yoyote anayetaka kuchanjwa akachanje kwa ajili ya kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo.
Na Ofisi ya waziri Mkuu, Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa rai kwa viongozi wa dini na waamini waendelee kuvumiliana, kustahamiliana na kushikamana katika kufanya ibada na kuienzi tunu ya amani. “Tuendelee kufanya ibada, kuwaombea wenzetu waliotangulia mbele za haki, tuoneshane upendo na mshikamano hata baada ya kumalizika kwa masiku haya kumi bora ya Dhul Hijja.” Waziri Mkuu ametoa rai hiyo Jumatano, Julai 21, 2021) katika Baraza la Eid El Adha lililofanyika katika Msikiti wa Mtoro, Ilala jijini Dar es Salaam. Amesema kila Mtanzania anapaswa kutambua kwamba anao mchango mkubwa katika kutunza na kuimarisha amani ya nchi, hivyo amewasihi wananchi wote waendelee kuitunza tunu hiyo. Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwasisitiza wananchi wote waendelee kuchukua hatua za kujikinga na Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19. “Tuendeleze tabia ya kunawa mikono mara kwa mara na maji safi yanayotiririka na sabuni na tukikosa maji tutumie vitakasa mikono. Tuvae barakoa zilizothibitishwa na mamlaka zetu.”
Waziri Mkuu amesema ni vema kwa sasa wananchi wakajiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima na wazingatie kukaa umbali wa mita moja au zaidi kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Amesema wananchi wanatakiwa wafanye mazoezi ya mara kwa mara kulingana na afya zao pamoja na mazingira yanayowazunguka, pia amewasihi wazingatie lishe bora. “Kwa wale wenye umri mkubwa na wenye uzito uliopitiliza na wenye magonjwa sugu kama moyo, pumu, kisukari na figo wanapaswa kuchukua hatua madhubuti zaidi kujikinga na ugonjwa huu.” Hata hivyo, Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi wawahi katika vituo vya kutolea huduma za afya mara waonapo dalili za mafua makali, maumivu ya koo, kichwa kuuma, kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula na kupoteza uwezo wa kunusa harufu mbalimbali.” Akizungumzia kuhusu chanjo ya Ugonjwa huo, Waziri Mkuu amesema chanjo hiyo ipo tayari nchini mwananchi yoyote anayetaka kuchanjwa akachanje kwa ajili ya kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa upande wake, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally amewataka watanzania kuendelea kuimarisha maadili mema yatakayoisaidia nchi yetu “Pia tumuombe Mwenyezi Mungu ili tuondokane na majanga yanayoikabili nchi yetu na ulimwengu mzima” Naye, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Sheikh Nuhu Jabir Mruma amesema baraza hilo linatoa wito kwa waislamu na Watanzania kwa ujumla waendelee kuienzi na kuilinda amani wanaposherehekea sikukuu ya Eid Al-Adh’haa. “Tunafanya hivi kwa kutambua kwamba amani ndio msingi wa maisha bora na yenye furaha kwa mwanadamu. Mwenyezi Mungu anatuelekeza juu ya faida ya amani katika kitabu chake kitukufu cha Qur’an sura ya 16 aya ya 112 na nanukuu “Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiufikia kwa nafasi kutoka kila mahali.”
Akizungumzia wimbi la tatu la ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19, Sheikh Mruma ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali hususan Wizara ya Afya kwa namna inavyochukua hatua za kukabiliana na kudhibiti janga hilo. Amesema hatua hizo zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali zimepunguza kwa kiasi kikubwa kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo nchini. “Tunawashukuru Watanzania kwa namna wanavyopokea, kutii na kuyafanyia kazi maelekezo ya viongozi katika kujikinga na kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo. Pia kiongozi huyo amesema baraza hilo linaendelea kuwahimiza Waislamu na wananchi kwa ujumla waendelee kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukuza uchumi. “Tunaamini kwa kufanya hivyo ndiyo tutakuwa tumeunga mkono kwa dhati juhudi za Serikali yetu katika kufikia malengo yake ambayo ni huduma bora kwa jamii yote.”
#Michezo Klabu ya Soka Simba SC sasa imetwaa ubingwa wa #ASFC kwa mara ya pili mufululizo Na ya Tatu katika historia ya michuwano iyo na ndio Klabu iliyo twaa mara nyingi zaidi
Simba imebeba ubingwa uho katika misimu ya 2016-17 2019-20 2020-21
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya (kulia).
kwenye ujenzi wa mradi wa stendi ya Mabasi ya Mangaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo hayo Julai 24, 2021 alipofanya ziara ya kustukiza katika stendi ya Mabasi ya Mangaka iliyopo Wilaya ya Nanyumbu na kukasirishwa na uongozi wa Wilaya kwa kufanya upotevu mkubwa wa fedha usiolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi huo.
Ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho Makamu wa Rais amesema hakilingani na ujenzi huo na ameagiza kupelekewa taarifa hizo ofisi kwake haraka iwezekanavyo.
Amesema viongozi hawana budi kusimamia fedha za serikali zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Timu zote zinakutanana kwenye Fainali ya #ASFC kwa mara ya kwanza Yanga SC bingwa mara Moja 2015-16 na Simba SC bingwa mara mbili 2016-17 na 2019-20 Yanga Wanasaka ubingwa wa 2 Simba Wanasaka ubingwa wa 3
Uamuzi wa Biden wa kuondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Afghanistan kufikia Septemba 11, 2021 umechukuliwa na mtazamo tofauti kote duniani.
Kuna wale wanachoshikilia kwamba ndio uamuzi stahiki na kudai imekuwa safari ndefu ambayo haikufanikiwa kufikia malengo yake ingawa pia kuna wakosoaji wake ambao wanachukulia kuwa hakukutolewa muda wa kutosha kwa Afghanistan kujitayarisha ipasavyo katika utekelezaji wa jukumu la kujilinda yenyewe kikamilifu.
Wakati huo Biden akiwa makamu rais, alikuwa anaunga mkono usaidizi wa kijeshi na kibinadamu kujenga tena Afghanistan baada ya Marekani kuondoa utawala wa serikali ya wanamgambo wa Taliban kwasababu ya kumuunga mkono kiongozi wa kundi la al- Qaeda Osama bin Laden, mratibu wa shambulizi la kigaidi lililotokea Septemba 11, 2001 nchini Marekani.
Kipindi hicho, Joe Biden alitembelea Afghanstani katika ziara rasmi kukutana na rais wakati huo Hamid Karzai kujadiliana hali nchini humo, lakini walitofautiana na kulingana na waliokuwa karibu, hafla ya chakula cha jioni ilikasitishwa ghafla bila kutarajiwa.
Bwana Biden alimaliza ziara yake akihisi kuwa vita vya Afghanistan ni kama mtego kwa Washington na huenda Marekani ikakosa kuvishinda.
Na aliporejea Marekani moja kwa moja alitoa onyo kali kwa aliyekuwa rais wakati huo Barack Obama kwamba »sasa sio wakati wa kuongeza wanajeshi wetu Afghanistan ».
Kipindi hiki ambapo Joe Biden ndio rais, ameamua kuondoa wanajeshi wake licha ya pingamizi kutoka kwa baadhi ya wataalam wa jeshi, wabunge wa Democratic na Republican na mafisa wa mashirika ya kutoa msaada.
Mtangulizi wa Biden, Donald Trump alifikia makubaliano na Taliban kwamba wanajeshi wote wa Marekani wataondoka nchini Afghanistan kufikia Mei mwaka huu na vyanzo vinasema kuwa Biden alikuwa na wasiwasi kwamba kukiukwa kwa makubaliano hayo huenda kungesababisha tena mashambulizi zaidi dhidi ya wanajeshi wa Marekani na kuwa sababu ya kuendeleza vita hivyo.
‘Raia wa Afghanistan waamue hatma yao’
.
Akitetea uamuzi wake, Rais Biden amekiri kuwa huenda kukazuka tena vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe huko Afghanistan lakini akarejelea kwamba nchi yake imejitolea kuondoa wanajeshi wake nchini humo huku Marekani ikiendeleza kuunga mkono usaidizi wa kidiplomasia na kibinadamu na kusisitiza kuwa hatma yao ipo mikononi mwao.
Raia wa Afghanistan, ni lazima waamue hatma yao badala ya kuweka kizazi kingine cha Marekani hatarini kwa vita ambavyo haiwezi kushinda ».
Biden alisema kuwa jeshi la Afghan lina uwezo wa kukabiliana na kundi la Taliban.
Vita hivyo vya muda mrefu ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa kipindi cha miaka 20, Biden alisema kuwa Marekani ilifikia lengo lake: ikiwa ni kukabiliana na kundi la wanamgambo wa Al-Qaeda na kuzuia mashambulizi zaidi dhidi ya Marekani kama lililotokea Septemba 11, 2011.
Mratibu wa shambulizi hilo, Osama bin Laden aliuliwa na timu ya wanajeshi wa Marekani mwaka 2011.
« Tulifikia malengo hayo, na hiyo ndio sababu tulienda huko. Hatukwenda Afghanistan kujenga taifa. Na ni haki na wajibu wa raia wa Afghan peke yao kuamua hatma yao na namna wanavyotaka kuendesha nchi yao, » Biden alisema.
Bwana Biden pia alitoa wito kwa nchi za eneo hilo kusaidia kuleta utulivu wa kisiasa kati ya pande zinazozozana. Alisema kuwa serikali ya Afghan inastahili kutafuta makubaliano na kundi la Taliban ili kuwezesha kuishi kwa amani kwa pamoja.
Timu za waokoaji nchini india zinajitahidi kupita katika maji machafu Jumamosi kufikia nyumba kadhaa zilizozama kwenye maji.
Vyanzo vya habari nchini humo vinasema idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi na ajali zilizosababishwa na mvua kubwa ya masika imeongezeka na kufikia 125.
Jimbo la Maharashtra limekumbwa na mvua kubwa zaidi mwezi Julai katika kipindi cha miongo minne, wataalamu wanasema.
Mvua hiyo iliyodumu kwa siku kadhaa imeathiri maelfu ya watu wakati mito mikubwa iko katika hatari ya kupasuka kingo zake.
Huko Taliye karibu kilomita 180 kusini mashariki mwa mji mkuu wa kibiashara Mumbai, idadi ya waliofariki iliongezeka na kufikia 42.
Takriban watu 40 bado wamekwama na uwezekano wa kuwaokoa wakiwa hai ni mdogo kwa sababu wamenasa kwenye tope kwa zaidi ya saa 36, afisa mmoja aliyekataa kutambulishwa amesema.
Mwanamuziki mashuhuri na kiongozi wa bendi ya Kilimanjaro Band, maarufu Njenje, nchini Tanzania Waziri Ally amefariki dunia.
Kulingana na wanafamilia Waziri alifariki baada ya kuugua ghafla na kuharakishwa katika hospitali ya Mwananyamala mjini Dar es salaam. Chanzo kamili cha kifo chake hakijaelezwa.
Waziri alikuwa kiongozi wa bendi ya Kilimanjaro kwa miaka mingi akishirikiana na wanamuziki wengine mashuhuru kama vile marehemu Mabruk “Babu Njenje” Hamisi, Mohamed Mrisho, Nyota Waziri, Keppy, John Kitime na wengineo
Waziri alianza kupiga muziki akiwa mdogo sana na bendi za muziki wa taarab mjini Tanga kama vile Lucky Star na Black Star. Uhodari wake wa kupiga kinanda ulimpa umaarufu hadi kuajiriwa na bendi za muziki wa dansi kama Nuta Jazz ya mjini Dar es salaam
Baadaye Waziri alijiunga na bendi ya vijana wenzake kutoka mjini Tanga, Kilimanjaro Band katika miaka ya 80 na kuanzia hapo hakutoka katika bendi hiyo hadi alipochukua uongozi wake katika miaka 90 baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo Hemed Chuky.
Waziri aliiongoza bendi ya Kilimanjaro katika mikataba mingi ya kimataifa iliyowawezesha kupiga muziki katika nchi za Japan, Uingereza na nchi Falme za Kiarabu.
Baada ya kutoa album ya Njenje, ambayo ilifanya bendi hiyo kujulikana kwa jina la Njenje – Kilimanjaro Band ilitoa album nyingine kadha zikiwa na nyimbo ziligonga chati kama vile Boko, Kinyaunyau, Kachiri, Tupendane, Ndembele, na Ndugu Zangu
Waziri wa Afya wa serekeli ya mapinduzi zanzibar #Nassor #Mazrui apatiwa chanjo ya kwanza ya Kinga ya virusi vya Corona iliyozinduliwa ijumaa visiwani humo
Watu kumi na sita wameuawa na wengine zaidi ya nane kujeruhiwa na waasi wanao dhaniwa kuwa wapiganaji wa kikundi chenye msimamo mkali wa kidini cha ADF ambao walishambulia lori moja la abiria.
Shambulizi hilo limetokea katika njia kuu kati ya miji ya Maimoya na Chani-chani, kiasi cha kilomita 40 kutoka mji wa Beni, jimbo la Kivu Kaskazini.
Lori hilo lilikuwa likitoka sokoni Pa Chanichani magharibi mwa Maimoya wilayani Beni kutoka Oicha , wengi wa waathirika wa mauaji hayo ni wanawake ambao walikuwa wakitoka sokoni kununua chakula.
Jeshi la Congo FARDC limefika eneo la tukio kutafuta mili ya watu iliyokuwa imefichwa porini na vile vile pikipiki zilizo shambuliwa na kuchomwa na waasi. Mili yote ilipelekewa Oicha Beni ili kusubiri matayarisho ya mazishi.
Shambulizi la kikundi cha waasi cha ADF nchini DRC
Shambulizi hili linakuja wakati ambapo Mkoa wa Kivu kaskazini unaongozwa na Gavana wa kijeshi ambaye yuko Beni.
Wananchi wanaelezea tukio hilo kuwa baya na kupoteza matumaini kwa hatua ya Rais Felix Tshisekedi aliyochukuwa kuweka viongozi wa kijeshi kumaliza uasi katika eneo hilo ambako watu zaidi ya elfu sita wameshapoteza maisha tangu 2013 hadi sasa
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.
Kauli hiyo imekuja baada ya kiongozi huyo wa upinzani kuwa anashikiliwa kwa takribani siku mbili, vyombo vya habari vimeripoti.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwamba, Mbowe alikamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza, jambo ambalo si kweli.
“Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika.
Hatua hiyo imefikiwa sasa,” alisema Misime.
Hivi karibuni Mbowe alifanya mkutano na waandishi wa habari na alikosoa kukamatwa kwa wafuasi wa chama hicho na polisi, pamoja na suala la mabadiliko ya katiba.
Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimesema hakitaendelea kumpigia magoti Rais wa nchi hiyo, Samia Hassan Suluhu kuhusu mustakabali wa taifa hilo, Mbowe aliwaambia waandishi wa habari hivi Jumatatu.
Kauli hii ya Mwenyekiti ilifuatia hatua ya Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuwakamata viongozi, wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi wa dini 38 waliokuwa wahudhurie mkutano wa chama hicho kupitia baraza lake la vijana (BAVICHA) wenye lengo la kuhamasisha kupatikana kwa katiba mpya ya nchi hiyo.
Jacky Ndala, kiongozi wa uongoziwa chama cha gavana wa zamani Moïse Katumbi amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa matamshi yake dhidi ya muswada unaojulikana ambao unakusudia kutoa nafasi pekee kwa raia wa nchi hiyo waliozaliwa na wazazi wote wazawa, kuwania nafasi kuu za uongozi, mswada ambao hata hivyo umewagawa wananchi wa Congo. Muswada huo, ikiwa utapitishwa na kutangazwa, unaweza kuwatenga wagombea kadhaa wa uchaguzi ujao wa urais, akiwemo kiongozi wake Moïse Katumbi, ambao hawakuzaliwa na wazazi wote wawili wenye uraia wa DRC. Jacky Ndala alikamatwa Jumapili asubuhi na maafisa wa idara ya ujasusi na kufikishwa masaa 24 baadaye kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa jamhuri huko Kinshasa-Matete. Alipofikishwa mbele ya majaji wa mahakama ya Amani ya Kinkole Jumanne, katika vitongoji vya Kinshasa, hatimaye alihukumiwa kifungo ha miaka miwili jela. Ikiwa Jacky Ndala amefikishwa mahakamani, ni kwa kwa sababu ya matamshi yake alioyatoa kwenye mkutano wake wa mwisho. Alitoa wito wa kuvamia makao makuu ya Bunge ikiwa muswada huo utapitishwa. Mwezi Julai mwaka jana, mbunge wa kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nsingi Pululu, aliwasilisha kwenye ofisi za Bunge muswada wa sheria ambao unakusudia kutoa nafasi pekee kwa raia wa nchi hiyo waliozaliwa na wazazi wote wazawa, kuwania nafasi kuu za uongozi. Kwa upande wa mwendesha mashtaka, anasema matamshi haya ni kosa « linalochochea utovu wa nidhamu kwa mamlaka ya umma ». Hata hivyo mwanasheria wa Jacky Ndala, wakili John Padou, anahoji hoja hii. « Kwetu, chanzo cha waraka huo kinatia shaka. Ibara hiyo inazungumza juu ya raia kupinga sheria, je! Hati ya Pululu ni sheria? Hapana. Ni pendekezo. Je! Ni sheria gani aliyodharau? … Hukumu hiyo ilitolewa pasikpo kuwa na kosa. Je! Ni marufuku kuandamana hadi makao makuu ya Bunge? Tutatumia njia za kisheria kukata rufaa kwa mujibu wa sheria za DRC ”.